Ofisa Masuala ya Bima wa NSSF, Peter Isack akitoa ufafanuzi kwa kuhusu majukumu ya kitengo chake kwa MkurugenziMkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto), wakati mkurugenzi huyo alipotembelea banda la NSSF katika maonyesho ya Sabasaba.
Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushto), juu ya viwanja vinavyouzwa na NSSF vilivyopo eneo la Kiluvya.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), akiangalia michoro ya nyumba ambayo ni sehemu ya miradi ya shirika hilo. Wa pili kulia ni Ofisa Uwekezaji wa NSSF, Moringe Nyerere.Jumamosi, 2 Julai 2016
MKURUGENZI MKUU NSSF AJIONEA MIRADI YA SHIRIKA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA 2016
Muonekano wa Banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), katika Maonyesho ya Biashara ya 40 ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa Mtoni Kijichi, Mohames Kimbe akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), kuhusu mradi wa nyumba za Kijichi. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Salim Kimaro na Juma Kintu kutoka Idara ya Uhusiano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (wa pili kulia), akiangalia mradi wa Mtoni Kijichi.
Ofisa Mauzo wa NSSF, Abbas Ramadhan akitoa maelezo kuhusu mradi wa nyumba wa Kijichi.
Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Salim Kimaro (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Aman Marcel wakimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara kifaa maalum kinachotumiwa na wanachama kutoa maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la NSSF.
Ofisa wa Masuala ya Bima
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni