Watu
20 wengi wao wakiwa ni raia wa kigeni wameuwawa katika shambulio
kwenye mgahawa nchini Bangladesh, linalodaiwa kufanywa na kundi la
Dola la Kiislam (IS).
Watu
wenye bunduki walivamiwa mgahawa huo wa Holey Bakery uliopo Jijini
Dhaka usiku wa wa manane Ijumaa kabla ya vikosi vya jeshi kufika saa
12 baadaye.
Washambuliaji
sita nao wameuwawa na mmoja amekamatwa maafisa wa Bangladesh
wameseam. Waziri Mkuu Sheikh Hasina ametangaza siku mbili za
maombolezo ya kitaifa.
Wageni
waliokufa ni pamoja na Waitalia tisa, Wajapan saba pamoja na raia wa
Marekani na raia wa India.
Polisi wakisaidiana kumbeba mtu aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo
Polisi akimsaidia askari polisi mwenzake aliyejeruhiwa katika mashambulizi hayo
Wanajeshi wakiwa kwenye vifaru wakiwasili eneo la tukio saa 12 baadaye
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni