.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 29 Agosti 2016

BMU YATEKETEZA ZANA ZA UVUVI HARAMU MASANZA.

                                                                 Na Shushu Joel, Rweyunga Blog - BUSEGA.

UONGOZI wa uangalizi wa mazingira ya mwalo katika kijiji cha Ijitu kata ya Kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu wameteketeza vyavu haramu aina ya makokolo kwa makusudi ya kuteketeza uvuvi haramu katika wilaya hiyo.

Akizungumza wakati wa uchomaji wa zana hizo Katibu wa Beach Management Unity( BMU) Adam Abel alisema kuwa makokolo ni nyavu ambazo ni hatari sana kwa mazalia ya viumbe viishivyo majini, kwani katika uvuvi wake ukokota kila kitu kilichoma ndani ya maji na hii inasababisha hasara kubwa kwa jamii husika na taifa kwa ujumla.

“Tumeamua kufanya hivi ili kuleta unafuu kwa wananchi na wavuvi wanatumia zana ambazo ni halali kwa jamii pia hii itaiongezea taifa pato kutokana na uzalishaji wa samaki wanaotakiwa kusafirishwa nje kuwa na tija na hata wale wadogo kukua bila kuwa na buguza ya aina yeyote ile”

Aliongeza kuwa makokolo yaliyochomwa ni mali ya Bi Yulitha Godfrey mkazi wa Bukome (37) ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za uvuvi haramu katika maeneo mbali mbali ya ziwa victoria.

Aidha katibu huyo alisema kuwa anawataka wale wote wanaotumia zana za uvuvi haramu wazisalimishe wenyewe katika ofisi za BMU ili kuwapunguzia buguza viongozi wao wa serikali kwani wanapaswa kutambua kuwa sasa hivi ukikamatwa na zana hizo unataifishwa na kila kitu ambacho ulikuwa ukitumia katika kazi zako za uvuvi huo haramu.

Abel pia amempongeza diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, Vumi Mgulila kwa ushirikiano ambao anawapatia katika kufanikisha agizo la Rais la kuteketeza zana haramu katika ziwa Victoria.

Kwa upande wake Yohana Peter ameupongeza uongozi huo kwa juhudi zake za kuhakikisha uvuvi haramu unatokomezwa katika wilaya ya Busega.

Aliongeza kuwa ili wafanikiwe zaidi, inawabidi wawashirikishe wananchi ili waweze kuwa wanawapa siri za wale wanaofanya uvuvi huo usiokubalika katika nchi.

Nyasato Maingu ni mfanya biashara mdogo wa samaki maarufu chinga ambaye ununua samaki kwa wavuvi na kisha kwenda kupima katika mizani anaeleza kuwa ni jambo la pongezi kwa Rais Magufuli kwa kutambua thamani ya ziwa pamoja na viumbe vilivyoma na hii itaifanya Tanzania kuongezeka kwa upatikanaji wa samaki kwa wingi kwani wale wadogo watakuwa hawavuliwi kiholela.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni