Mshambuliaji
Diego Costa ameifungia goli la ushindi Chelesa kwa mara ya pili
katika michezo miwili mfululizo baada ya kutoka nyuma kwa goli moja
hadi kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Watford.
Watford
walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Eyienne Capoue na kuifanya
kuongoza katika dakika ya 56, wakati wenyeji hao wakionekana
kuumiliki mchezo huo katika dimba la Vacarage Road.
Hata
hivyo mchezaji aliyetokea benchi Michy Batshuayi alisawazisha goli la
kwanza kwa Chelsea tangu ahamie klabu hiyo, na kisha baadaye Diego
Costa aliikimbilia pasi ya Cesc Fabregas na kumfunga kwa tobo kipa
Heurelho Gomes.
Michy Batshuayi akishangilia goli lake la kwanza akiwa na Chelsea
Diego Costa akiifungia Chelsea goli la ushindi
Wakati
huo huo Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City na
walioshika nafasi ya pili Arsenal wameshindwa tena kupata ushindi wao
wa kwanza katika msimu huu baada ya kutoka sare tasa katika dimba la
King Power.
Kipa Cech akijiandaa kudaka mpira uliopigwa na Jamie Vardy





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni