Imamu
na msaidizi wake wameuwawa kwa kupigwa risasi wakitembea mtaani wakati wakitoka msikiti Jijini New York nchini Marekani.
Msemaji
wa polisi amesema wawili hao walifuatiliwa kwa nyuma na mwanaume
mmoja aliyewapiga risasi vichwani.
Imamu
Maulama Akonjee, 55, alihamia mji huo akitokea Bangladesh miaka
miwili iliyopita kwa mujibu wa ripoti za Jijini New York.
Polisi
wamesema kuwa hakuna ripoti zinazoashiria kuwa Imamu huyo na msaidizi
wake walishambuliwa kutokana na imani yao.
Waumini wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kupata taarifa za kifo cha Imamu wao na msaidizi wake
Waumini wakipaza sauti zao kutaka haki itendeke kufuatia vifo hivyo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni