Mwanariadha
wa Uingereza Mo Farah mwenye asili ya Somalia amefanikiwa kutetea
ubingwa wa mbio za mita 10,000 katika michuano ya Olimpiki na kutwaa
medali ya dhahabu.
Katika
mbio hizo Farah alijikuta akianguka katika raundi ya 10 baada ya
kukwatuliwa kwa bahati mbaya na mwanariadha mwenzake Galen Rupp,
lakini alinyanyuka na kuendelea.
Mwanariadha
wa Kenya Paul Tanui alipambana vilivyo na kumpita Farah, lakini
bingwa huyo alizidisha kasi na kumpita. Farah anakuwa Muingereza wa
kwanza kushinda medali tatu za dhahabu za Olimpiki.
Mo Farah akishangilia ushindi baada ya kufanikiwa kuibuka mbabe wa mbio za mita 10,000
Mo Farah akiwa amepiga magoti na kumshukuru Mungu kwa ushindi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni