Neymar
amefunga goli lake la kwanza wakati wenyeji wa michuano Olimpiki timu
ya Brazil wakiwafunga Colombia kwa magoli 2-0 na kutinga nusu fainali
ya michuano hiyo kwa mchezo wa soka.
Mshambuliaji
huyo wa timu ya Barcelona alipiga mpira wa adhabu wa kuzungusha na
kupachika goli katika dakika ya 12, na kisha Luan aliongeza la pili
katika kipindi cha pili kwa shuti zuri la kunyanyua mpira juu uliojaa
wavuni.
Kwa
ushindi huo Brazil sasa watacheza na Honduras katika mchezo wa nusu
fainali, baada ya Honduras kuifunga Korea Kusini goli moja kwa bila
lililopachikwa na Albert Elias. Ujerumani itaavaana na Nigeria.
Mpira uliopigwa na Luan ukijaa wavuni na kuandika goli la pili la Brazil
Refa akimpatia kadi ya njano Neymar baada ya kumchezea rafu mchezaji wa Colombia
Mchezo huo uligubikwa na matukio ya wachezaji kutishiana kuonyeshaba ubabe kama inavyoonekana hapa




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni