Eden
Hazard ambaye ameanza msimu huu akiwa kwenye kiwango kizuri
ameifungia Chelsea goli moja katika ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya
Burnley.
Katika
mchezo huo Hazard alikuwa wa kwanza kufunga goli kwa shuti la
kuzungusha, kabla ya Willian kuongeza la pili, na kisha Victor Moses
kufunga goli la tatu.
Eden Hazard akiachia shuti la kuzungusha lililojaa wavuni
Victor Moses akifunga goli la tatu la Chelsea
Katika
mchezo mwingine Liverpool imejikuta ikilazimwishwa sare ya goli moja
kwa moja na Tottenham Hotspur, katika dimba la White Hart Lane.
Liverpool
ilipata goli lake la kwanza kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Milner baada ya Erik Lamela
kumfanyia madhambi Roberto Firmino.
Tottenham walipambana kiume wasiaibishwe nyumbani na alikuwa Danny Rose
aliyesawazisha goli katika kipindi cha pili
Milner akijipinda na kuachia shuti la mkwaju wa penati na kuifungia Liverpool goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni