Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza timu ya Leicester City wamepata
ushindi wao wa kwanza wakiwa nyumbani baada ya kuifunga Swansea
magoli 2-1.
Leicester
City walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Jamie Vardy kisha baadaye Wes
Morgan akaifungia goli la pili.
Riyad
Mahrez alikosa penati baada ya Shinji Okazaki kufanyiwa rafu. Katika
kipindi cha pili Swansea ilicharuka na alikuwa Leroy Fer aliyeifungia
goli pekee mpira wa kichwa.
Jamie Vardy akiachia shuti lililoandika goli la kwanza la Leicester City
Leroy Fer akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliozaa goli pekee la Swansea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni