.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 13 Agosti 2016

LIGI KUU YA UINGEREZA: LEICESTER CITY WAANZA KWA KUPEWA KIPIGO

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City wameianza ligi hiyo kwa kuduwaza na kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa timu iliyopanda daraja ya Hull City.

Kikosi cha kocha Mike Phelam kiliongoza kwa kufunga goli lililofungwa kwa pamoja na wachezaji Adama Diomande na Abel Hernandez hata hivyo goli hilo alipewa Diomande.

Goli hilo lilizawazishwa baadaye na Riyad Mahrez kwa njia ya penati baada ya mchezaji mpya wa Leicester City Ahmed Musa kufanyiwa madhambi.

Hull City ilipata goli la pili na la ushindi kupitia kwa Robert Snodgrass baada ya krosi aliyoipiga kushindwa kuzuiliwa na mabeki.
   Goli la Hull City lililofungwa na wachezaji wawili Adama Diomande na Abel Hernandez 
  Riyad Mahrez akipongezwa na wenzake baada ya kufunga goli kwa mkwaju wa penati
     Robert Snodgrass akishangilia goli la pili na la ushindi kwa Hull City alilofunga 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni