Madaktari wa wanyama nchini Thailand
wamemfanyia upasuaji nyoka mkubwa aina ya anaconda mwenye umri wa
miaka 10 na kufanikiwa kuondoa uvimbe uliokuwa karibu na moyo wake.
Nyoka huyo alipewa dawa za usingizi
katika upasuaji huo uliofanyika kwa muda wa saa saba, Dk. Taweesak
Anansiriwattana wa hospitali ya wanyama ya Klongluang ameliambia
shirika la habari la BBC.
Madaktari hao waliupasua mwili wa
nyoka huyo na kuutoa uvimbe wa kilo 1, na kisha kuchukua sambuli zake
kwa ajili ya vipimo vya kimaabara ili kubaini iwapo nyoka huyo
alikuwa na saratani.
Nyoka anaconda akiwa amewekewa mirija ya oxygen mdomoni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni