Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Philippine amesema zaidi ya watu 1,900 wameuwawa wakati wa msako
dhidi ya biashara za dawa za kulevya katika muda wa wiki saba
zilizopita.
Mkuu huyo Ronald dela Rosa ametoa
maelezo hayo mbele ya baraza la seneti kuhusiana na ongezeko kubwa la
mauaji tangu rais Rodrigo Duterte awe rais wa nchi hiyo.
Amesema kuwa operesheni za polisi
zimeuwa watu 750, lakini vifo vingine bado vinafayiwa uchunguzi.
Rais Duterte alishinda urais akiwa
na sera zake za msimamo mkali za kutokomeza biashara ya dawa za
kulevya.
Rais wa Philippine Rodrigo Duterte
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni