.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 23 Agosti 2016

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI APOKELEWA KWA MABANGO ITILIMA

Na Shushu Joel,SIMIYU . WANANCHI wa kijiji cha Mahembe kata ya Sawida wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wamempokea kwa mabango Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Medadi Kelemani wakati alipokwenda kuwatembelea wakazi hao ili kubaini kero zao katika upande wa sekta yake.
 

Julius Limbe ni mkazi wa kijiji hicho anaeleza kuwa ni miaka mingi sana kwa wakazi wa eneo hilo hawajawahi kuona hata umeme wala maji na hata barabara, na hivyo kujihisi kuwa wako katika sayari nyingine kabisa katika ulimwengu huu.

Akijibu maswali na kero za wananchi hao, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dr Kalemani amewataka wananchi hao kuwa na subira kwani hawamu hii ya tano si ya mchezo bali ni ya vitendo kwa kwenda mbele.

Aliongeza kuwa kuhusu umeme kuna REA awamu ya tatu inakuja ambayo itakuwa ni kila kijiji kuwa na umeme katika nchi yetu hivyo amewataka wananchi hao pindi umeme huo utakapoanza kuwekwa katika vijiji hivyo wanapaswa kujitokeza kuvuta umeme ndani ya majumba zao kwa kiasi cha shilingi elfu 27 tu.

Kuhusu mahitaji mengine amesema kuwa atayafikisha sehemu husika ili yaweze kufanyiwa kazi kwa haraka na uharaka zaidi.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni