Timu
ya Manchester City imeendeleza wimbi la ushindi na kuongoza Ligi Kuu
ya Uingereza kwa tofauti ya idadi ya magoli baada ya kuifunga West
Ham kwa magoli 3-1.
Katika
mchezo huo Manchester City walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia
kwa Raheem Starling na kisha baadaye Fernandinho aliongeza la pili
kwa mpira wa kichwa.
Michail
Antonio alipunguza tofauti ya magoli baada ya kuifungia West Ham
katika kipindi cha pili, kabla ya Sterling kufunga la tatu katika
dakika ya 90.
Fernandinho akiruka juu na kupiga mpira wa kichwa uliozaa goli la pili la Manchester City.
Timu
ya Middlesbrough imeendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika Ligi Kuu
ya Uingereza baada ya kutoka sare tasa na timu ya West Brom hii leo.
Katika
mchezo huo beki wa kushoto Brendan Galloway alipata nafasi nzuri ya
kufunga katika kipindi cha kwanza baada ya kupanda mbele lakini kipa
wa Middlesbrough Brad Guzan alikuwa imara.
Kipa Brad Guzan akizuia mpira uliopigwa na James McClean
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni