Timu
ya West Ham ya Uingereza imeinasa saini ya mshambuliaji wa Italia
Simone Zaza akitokea Juventus kwa mkopo wa msimu mzima wa kiasi cha
paundi milioni 4.3.
Makubaliano
hayo ya kumtwaa Zaza yanaweza kuwa ya kudumu na kufikia ada ya paundi
milioni 17, na nyongeza ya milioni 2.5 kulingana na atakavyokuwa
anashuka dimbani.
Usajili
huo ni wa 11 kwa West Ham katika majira ya joto, na umefikisha kiasi
cha paundi milioni 60 zilizotumika kwa usajili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni