Wadhamini wanne wamemtosa muogeleaji
wa Marekani mzushi, Ryan Lochte, wakiwemo watengenezaji wa Speedo na
kampuni ya mavazi ya Ralph Lauren.
Uamuzi huo umekuja baada ya kampuni
ya bidhaa za ngozi ya Syneron-Candela na ya Japan ya kutengeneza
magodoro ya Airweave nao kujitoa kumdhamini Lochte.
Hatua hiyo ya wadhamini kumtosa
Lochte inafuatia kitendo chake cha kudanganya kuwa ameibiwa kwa mtutu
wa bunduki na polisi usiku akiwa Rio wakati wa Olimpiki.
Lochte, ambaye ameshinda mara 12
medali za dhahabu za michuano ya Olimpiki amekuwa akichuma mamilioni
ya dola kutoka kwa wadhamini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni