Kocha wa Leicester City, Claudio
Ranieri, amesema kuwa kocha Jose Mourinho ni mtu mzuri, na misuguano
yao yoyote ya nyuma imebakia historia.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya
Uingereza wataivaa Manchester United katika dimba la Old Trafford
hapo kesho, huku makocha hao wakiwa na historia ya kukorofishana.
Jose Mourinho aliwahi kumuita
Ranieri mtu aliyeshindwa wakati alipochukua nafasi yake Chelsea na
pia alimtolea lugha chafu akiwa kocha wa Inter Milan.
Kocha Jose Mourinho amekuwa na tabia ya kubwatuka na kukorofishana na makocha wenzake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni