Imebainika kuwa mzozo wa maneno
baina ya Brad Pitt na mtoto wake Maddox ndio uliomfanya Angelina
Jolie kufungua madai ya kuomba talaka mahakamani.
Tukio hilo linafanyiwa uchunguzi na
FBI, lakini moja ya chanzo kimesema tuhuma za kumpiga mtoto huyo
zimetiwa chumvi.
Hapo jana polisi wameonekana
wakiwasili kwa gari kwenye nyumba ya Jolie na Pitt iliyopo Hollywood Hills, ambako Pitt
inasemekana anakaa kwa wakati huu.
Muigizaji filamu Brad Pitt akiwa na mtoto wake wa kuasili Maddox
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni