.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 5 Septemba 2016

KOCHA WA UINGEREZA SAM ALLARDYCE AMPA UHURU WAYNE ROONEY KUCHEZA POPOTE

Kocha wa Uingereza Sam Allardyce amesema si jukumu lake kusema Wayne Rooney acheze nafasi gani, kauli aliyoitoa wakati akipata ushindi wa kwanza wa goli 1-0 dhidi ya Slovakia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe.

Katika mchezo huo Uingereza ilipata tabu kupata ushindi dhidi ya Slovakia iliyobakia na wachezaji 10, kabla ya Adam Lallana kuipatia ushindi wa sekunde chache kabla ya kipenga cha kumaliza mchezo.

Katika mchezo huo Rooney amefikisha michezo 116 kushinda akiwa ni kapteni wa Uingereza, ambapo kwa jana alijikita zaidi katika kucheza nafasi ya kiungo.
                                                               Kapteni Wayne Rooney akiwa kibaruani
                      Mpira uliopigwa na Adam Lallana ukitinga wavuni na kuandika goli pekee

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni