Mlipuko unaodhaniwa kuwa ni wa bomu
umetokea usiku wa jumapili huko Manhattan na kujeruhi watu 29.Polisi Jijini New York wanachunguza kitu kingine kinachodhaniwa kuwa ni bomu la pili lililopo kwenye chombo cha kupikia maarufu kwa lugha ya kigeni kama pressure cooker.
Picha za CCTV zenye kuogofya
zinaonyesha mlipuko huo ukitokea New York katika eneo la jirani na
Chelsea majira ya saa mbili na nusu usiku.
Mtu aliyejeruhiwa akiwa kwenye machela yenye magurudumu akiwahishwa kupatiwa matibabu
Mmoja wa majeruhi akiwa amepatiwa huduma ya kwanza kwenye gari la wagonjwa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni