JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail:
press@ikulu.go.tz
Tovuti :
www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amewahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa atasimamia kwa nguvu zote
masuala yote yanayohusu maendeleo, kudumisha Muungano wa Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar na kudumisha amani kwa faida ya wananchi.
Rais
Magufuli amesema hayo leo tarehe 03 Septemba, 2016 alipokuwa
akizungumza na wananchi wa Zanzibar katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa Kibandamaiti Mjini Unguja.
Dkt.
Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amesema ili
mambo hayo yafanikiwe Wananchi wa Zanzibar hawana budi kukataa
kujihusisha na vitendo vya vurugu na kuvunja amani na amewaonya watu
wanaochochea vitendo hivyo kuacha mara moja.
Amewataka
wananchi wa Zanzibar kujihadhari dhidi ya wanasiasa ambao
wanapandikiza chuki, ubaguzi na fitina, kwani watu hao wanataka
kubomoa misingi mizuri ya umoja, upendo na mshikamano wa Taifa
uliojengwa na waasisi wa Taifa hili.
Rais
Magufuli amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein aliyehudhuria mkutano huo, kwa hatua
mbalimbali anazozichukua kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar
huku akibainisha kuwa tatizo la maji linalovikabili visiwa vya
Zanzibar litakwisha baada ya kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa maji
utakaofadhiliwa na Serikali ya India kwa gharama ya Dola za Marekani
Milioni 92, na mradi mwingine utakaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya Dola za Marekani Milioni 21.
Aidha,
Rais Magufuli amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi
nzuri vinayofanya katika kusimamia amani visiwani humo huku
akivihakikishia kuwa yeye akiwa kiongozi wao anawaunga mkono.
Pamoja
na Rais Shein Mkutano huo umehudhuriwa na Mke wa Rais wa Kwanza wa
Zanzibar Mama Fatma Karume, Mawaziri na Viongozi wa Siasa na Dini.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja
03
Septemba, 2016
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni