.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 6 Septemba 2016

WAFANYAKAZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WATINGA MAHAKAMANI

Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko.

                                                                                            Na Woinde shizza,Arusha

Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),  wamefungua kesi kumshtaki Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo  kwa madai ya kuvunja mikataba ya ajira.

Kesi hiyo wameifungua katika Mahakama ya Haki ya Jumuiya  ya Afrika Mashariki (EACJ) kitengo cha awali.

Wafanyakazi watatu kutoka Idara ya Amani na Usalama  Katibu Mkuu huyo alivunja mikataba yao ya ajira kinyume na agizo la Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliyoyatoa kwenye mkutano wa nyongeza
wa 31 na kwa kuzingatia Kanuni ya 96 ya taratibu za wafanyakazi wa EAC ya mwaka 2006.

Wanadai kuwa walipokea barua kutoka Masjala ya EAC yenye notisi ya miezi mitatu ya kusitishwa kwa ajira zao iliyowekwa saini na katibu mkuu huyo, huku ikieleza kuwa EAC haina fedha za kuendeleza mradi wa APSA unaopata fungu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Umoja wa Afrika (AU).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni