Wafungwa wanaoshikiliwa na kundi la
Dola ya Kiislam (IS) wameuliwa kikatili kwa kupigwa mawe kwa kudaiwa
kufanya kosa la kuzini.
Picha zinazotisha zinawaoyesha
watuhumiwa hao wakiwa wamefungwa macho na kitambaa wakipigwa mawe
katika mji wa Abu Kamal mashariki mwa Syria, karibu na mpaka na Irak.
Mamia ya watu wakiwemo watoto
wanaonekana katika eneo la kati la mji huo wakati wafuasi wa IS
wakitekeleza adhabu hiyo hadharani.
Mawe yakiwa yamebebwa kwenye gari kwa ajili ya kutumika kutekeleza adhabu hiyo
Mamia ya watu wakishuhudia adhabu hiyo ya kuuwawa kwa kupigwa mawe kwa wazinifu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni