Mrembo
mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya
kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga
uwanja wa michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo
Vingunguti jijini.
Akizungumza katika Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.
Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.
Jokate ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.
“Nashukuru kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.
Alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.
Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia viwanja vya shule jirani katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni moja ya masomo muhimu sana.
Ngozi alisema kuwa wanatambua kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule yao, lakini kutokana na kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.
“Tunashukuru Jokate kwa ahadi ya kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo, hii itatoa hamasa kwa wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali kutambuliwa na vile vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la utawala, samani za ofisini na kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau watusaidie kufanikisha hayo,” alisema Kasango.
Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kati ya wanafunzi zaidi ya 290 wanaomaliza kidato cha nne, Kkhalid Ibrahim alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora huku Latifa Kihiyo akitwaa tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni