Mario Balotelli mpya amendelea
kuonyesha makali yake na kuisaidia Nice kuibuka na ushindi wa magoli
4-1 dhidi ya Nates, na kuifanya timu yake kuongoza Ligi 1 kwa tofauti
ya pointi sita.
Mshambuliaji huyo wa Italia,
aliyejiunga na Nice akitokea Liverpool, alifunga goli sita katika
ligi hiyo na pia kusaidia kupatikana mengine mawili akitakata mno
katika dimba la Allianz Riviera.
Kiungo Wylan Cyprien alitikisa nyavu
mara mbili na Alassane Plea naye alifunga goli na kuifanya Nice
ambayo haijafungwa kuwa na pointi 29 katika michezo 11.
Wylan Cyprien akifunga goli la kwanza la Nice
Super Mario Balotelli akifunga goli huku kipa wa Nates akiwa hana jinsi zaidi ya kuuangalia mpira uliomshinda kuudaka ukitinga wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni