Kocha wa Manchester City Pep
Guardiola amekanusha madai kuwa amewaambia wachezaji wake kutofanya
tendo la ndoa baada ya saa sita usiku.
Kiungo Samir Nasri, ambaye anachezea
kwa mkopo timu ya Sevilla, alidai kuwa kocha Guardiola alitoa agizo
hilo ili wachezaji wapate muda wa usingizi mzuri.
Hata hivyo kocha huyo wa zamani wa
Barcelona, amekanusha madai hayo na kusema yeye anawahamasisha
wachezaji wake wafanye zaidi tendo la ndoa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni