Wananchi wengi wa India wamejitolea
kumchangia figo Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Bi. Sushma Swaraj
baada ya kutwitti anafanyiwa vipimo vya kupandikiziwa figo.
Bi. Swaraj mwenye umri wa miaka 64,
amekuwa na historia ya kuugua kisukari na alikuwa amelazwa kwenye
hospitali huko Delhi, mapema mwaka huu.
Bi. Swaraj ni mmoja wa mawaziri
wenye uzoefu wa juu katika serikali ya Waziri Mkuu wa India Narendra
Modi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni