Goli la kusawazisha la Olivier
Giroud la dakika ya 89, limeipatia Arsenal pointi moja na kuinyima
Manchester United ushindi ambao walikuwa wakishahili kuupata katika
dimba la Old Trafford.
Katika mchezo huo Juan Mata
aliifungia Manchester United goli la kwanza kwa shuti la guu la
kushoto, akiunganisha pasi ya Ander Herrera katika dakika ya 68.
Arsenal walikuwa hawajafanya
jitihada zozote makini za kutafuta goli walijikuta wakisawazisha goli
hilo kupiti Giroud aliyeunganishwa kwa kichwa krosi ya Alex
Oxlade-Chamberlain.
Kipa Petr Cech akiwa hana la kufanya baada ya kushindwa kuzuia shuti la Juan Mata
Mshambuliaji Oliver Giroud akiwa ameruka juu na kupiga mpira kwa kichwa uliosawazisha goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni