Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick
yake ya 39 katika maisha yake ya soka, na kuiongoza Real Madrid
kuwafunga wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid magoli 3-0 na
kujikita kileleni mwa ligi ya La Liga.
Mshambuliaji huyo Mreno alifungua
mvua ya magoli kwa kufunga kwa shuti la mpira wa adhabu lililogongwa
na kumpoteza mahesabu golikipa wa Atletico Madrid Jan Oblak.
Ronaldo tena akaongeza la pili kwa
mkwaju wa penati na kisha baadaye akatikisa goli la tatu akitumbukiza
kimiani krosi ya Gareth Bale.
Real Madrid sasa wanaongoza La Liga
kwa tofauti ya pointi nne, dhidi ya anayemfuatia Barcelona, ambao
walidhibitiwa na kutoka sare taza na Malaga katika mchezo wa mapema
jana.
Cristiano Ronaldo akifunga goli la kwanza kwa shuti la mpira wa adhabu
Cristiano Ronaldo akishangilia goli lake la tatu huku kipa wa Atletico Madrid akiwa kakaa chini mpira ukiwa wavuni
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni