Timu za Liverpool, Manchester City
na Paris Saint-Germain zimeonyesha jeuri ya fedha kwa kuamua
kuchangia paundi 120,000 za usafiri binafsi wa ndege kwa nyota wao wa
timu ya taifa ya Brazil.
Gharama za ndege hiyo ya kukodi
ilichangiwa na klabu hizo ili kuwawezesha wachezaji wao kurejea
kwenye klabu zao kwa wakati ili kujiandaa na michezo ya ligi, baada
ya kulitumikia taifa lao la Brzail.
Wakati ndege hiyo ikitua Uingereza,
wachezaji wa Brazil wa timu ya Chelsea walikuwa bado wapo Amerika ya
Kusini baada ya Brazil kushinda magoli 2-0 dhidi ya Peru huko Lima,
ambapo walikuwa wanangojea usafiri wa ndege wa kuunga unga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni