Manchester United wanamfuatilia kwa
karibu mshambuliaji kinda wa Celtic, Moussa Dembele, na kunauwezekano
wakamsajili Januari, mwakani.
Timu hiyo yenye maskani yake Old
Trafford imemtuma msaka wachezaji David Friio kumuona Dembele, 20,
wakati akiifungia Ufaransa magoli mawili katika mchezo dhidi ya
Uingereza U21.
Kocha Jose Mourinho inaeleweka
amekuwa ni shabiki wa Dembele na ameshamuangalia mchezaji huyo
akicheza mara tatu katika msimu uliopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni