Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza
Chelsea wamefikia rekodi ya kushinda mechi 13 mfululizo baada ya
kuibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Stoke City katika dimba la
Stamford Bridge.
Kipindi cha pili kilichokuwa na
mpira wenye kuburudisha kilishuhudia goli tano zikifungwa ambapo
Chelsea ililazimika mara mbili kuongeza goli ili iongoze.
Gary Cahill aliipatia Chelsea goli
la kuongoza kabla ya mapumziko, lakini beki wa Stoke Bruno Martins
Indi alisawazisha goli.
Willian aliifanya Chelsea iongoze
tena lakini Peter Crouch akaisawazishia tena Stoke, hata hivyo
Willian aliongeza la tatu na kisha baadaye Diego Costa akafunga goli
la nne.
Beki Gary Cahill akifunga goli la kwanza kwa mpira wa kichwa
Bruno Martins Indi akifunga goli la kusawazisha la Stoke
Diego Costa akifunga goli la nne la Chelsea na kufanya matokeo kuwa 4-2
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni