.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 1 Januari 2017

LEICESTER CITY YAENDELEA KUKIMBIA KUNDI LA KUSHUKA DARAJA

Leicester City imeongeza pointi sita juu ya mstari wa kushuka daraja, baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya West Ham United.

Alikuwa Slimani ambaye awali mpira alioupiga kwa kichwa uliishia kugonga mwamba, ndite aliyeifunga goli pekee akiunganisha mpira wa krosi nzuri ya Marc Albrighton.
                          Slimani akiwa juu baada ya kupiga kichwa mpira ambao ulienda kujaa wavuni 
Wakati huo huo Andre Gray amekuwa mchezaji wa kwanza wa Burnley kufunga magoli matatu 'hat-trick' katika ligi kuu ya Uingereza wakati wakiibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Sunderland.

Gray, lifunga goli lake la kwanza kufutia kujichanganya kwa mabeki John O'Shea na Papy Djilobodji, kisha akafunga goli la pili kwa kumzunguka Vito Mannone na kufunga la tatu kwa shuti kufuatia pasi ya Ashley Barnes.
             Andre Gray akiachia shuti na kufunga goli lake la kwanza katika mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni