Mchezaji wa Leicester City
aliyetokea benchi Ahmed Musa alifunga magoli mawili na kuisaidia
kusonga raundi ya nne ya kombe la FA kwa kuifunga Everton magoli 2-1.
Katika mchezo huo Everton iliongoza
kwa goli lililofungwa na Romelu Lukaku aliyeunganisha krosi ya Gerard
Deulofeu katika dakika ya 63.
Musa aliyeingia kuchua nafasi ya
Leonardo Ulloa, alisawazisha goli ndani ya dakika tatu tangu aingie
dimbani na kisha kushirikiana vyema na Danny Drinkwater na kufunga la
pili.
Mshambulaji Romelu Lukaku akiifungia Everton goli
Ahmed Musa akifunga goli lake la kwanza kati ya mawili aliyofunga jana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni