Kapteni wa muda Olivier Giroud
ameifungia Arsenal goli la ushindi, baada ya timu hiyo kutokea nyuma
katika mchezo wa raundi ya tatu wa kombe la FA, na kusonga mbele
katika raundi ya nne.
Timu ya Preston iliwashtua wageni
Arsenal kwa kufunga goli la kwanza kupitia kwa Callum Robinson na
kisha baadaye nusura waongeze la tatu.
Hata hivyo Ramsey katika dakika ya
kwanza ya kipindi cha pili kwa kuwapita mabeki wawili na kuachia
shuti lililojaa wavuni. Giroud akafunga goli la pili na kufanya
matokeo kuwa 2-1.
Ramsey akiwa amejipinda kuachia shuti lililozaa goli la kusawazisha
Olivier Giroud akifunga goli la pili katika dakika ya 88 ya mchezo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni