.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 3 Januari 2017

MANCHESTER UNITED YAFUNGANA POINTI NA TOTTENHAM SPURS KATIKA NAFASI YA TANO

Manchester United imefungana pointi na timu ya Tottenham katika nafasi ya tano baada ya kupata ushidi dhidi ya West Ham iliyobakia na wachezaji 10 baada ya kutolewa kiutata mchezaji wao Sofiane Feghouli.

Katika mchezo huo refa Mike Dean alimuonyesha Feghouli kadi nyekundu baada ya kiungo huyo kumkaba Phil Jones katika dakika ya 15, na kuonekana kama amemchezea rafu lakini haikuwa hivyo.

Antonio Valencia alijikuta akijuta kukosa nafasi ya kufunga goli katika kipindi cha pili, kabla ya Juana Mata kufunga goli kwa shuti la umbali wa yadi 10, baada ya kupata pasi kutoka kwa Marcus Rashford. Zlatan Ibrahimovic aliongeza goli la pili.
                             Juan Mata akiwa ameshatikisa nyavu na kuandika goli la kwanza
                Zlatan Ibrahimovic akifunga goli ambalo ilionekana kaotea lakini refa akalikubali

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni