.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 16 Januari 2017

SENEGAL YAWA TIMU YA KWANZA KUPATA USHINDI KATIKA MICHUANO YA AFCON

Senegal imeanza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya timu ngumu ya Tunisia.

Tunisia nusura wapate goli la kuongoza katika dakika ya pili mpira wa kichwa wa Ahmed Akaichi kugonga mwamba na kisha kupiga shuti nje.

Senegal ilipata goli la kuongoza kupitiwa kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Sadio Mane baada ya Cheikhou Kouyate kuangushwa chini.

Kara Mbodj alifunga goli la pili kwa kicha cha nguvu, huku Tunisia wakipoteza nafasi nyingi ikiwamo ya Youssef Msakni aliyepiga nje mpira wa kichwa.
                                   Sadio Mane akishangilia baada ya kufunga goli la mkwaju wa penati.

Katika mchezo wa awali hapo jana Algeria ilijikuta ikilazimisha kutoka sare na Zimbabwe ya magoli 2-2 dhidi ya Zimbabwe, huku Riyad Mahrez akifunga magoli yote mawili.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni