Wakazi wa kaunti ya Kirinyaga nchini
Kenya wamekumbwa na hofu ya kuwa huenda wamekuwa wakilishwa nyama ya
punda baada ya kuonekana mabaki ya vichwa vya punda katika maeneo
kadhaa ya kaunti hiyo.
Mkazi wa kaunti ya Kirinyaga katika
kijiji cha Murubara Bi, Wariara Githinji amesema wameshangazwa
kubaini vichwa vinne vya punda vikiwa vimetelekezwa katika eneo
mabalo wanyama hao wamechinjwa.
Vichwa hivyo na mabaki mengine ya
punda ikiwemo utombo vilibanika na watoto waliokuwa wakienda shule
ambao walikuwa wakishangaa hali iliyowavuta watu wazima waliokuwa
wakipita njia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni