Argentina imepata pigo katika mbio
za kuwania kufuzu kutinga fainali za kombe la dunia baada ya kukubali
kipigo cha magoli 2-0 dhidi ya Bolovia.
Katika mchezo huo Argentina ilimkosa
mshambuliaji wao nyota Lionel Messi baada ya kupewa adhabu ya kukosa
michezo minne kwa kumtukana mwamuzi.
Adhabu hiyo ya Messi imetokana na
kitendo cha kumtukana mwamuzi msaidizi Alhamis katika mchezo
walioshinda kwa goli 1-0 dhidi ya Chile.
Juan Carlos Arce na Marcelo Martins
waliifungia Bolivia, huku beki wa Everton Ramiro Funes Mori alijikuta
akitolewa nje kwa machela baada ya kuumia.
Mchezaji Juan Carlos Arce akishangilia goli alilofunga
Marcelo Martins akiupiga mpira kwa kichwa na kufunga goli la pili



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni