Teknolojia ya video imetumika
kurekebisha maamuzi ya makosa ya waamuzi katika mchezo wa kimataifa
wa kirafiki ambao Hispania iliifunga Ufaransa magoli 2-0 Jijini
Paris.
Mshambuliaji wa Ufaransa Antoine
Griezmann goli lake lilikataliwa kwa msaada wa teknolojia ya video
kutokana na kuotea.
Goli la pili la Hispania
lililofungwa na Gerard Deulofeu, lilikubaliwa na teknolojia ya video
baada ya mshika kibendera kuashiria kimakosa kuwa ameotea.
David Silva aliifungia Hispania goli
la kwanza kwa mkwaju wa penati baada ya Laurent Koscielny kumchezea
rafu Deulofeu.
Gerard Deulofeu akifunga goli lililokataliwa na mshika kibendera lakini likakubaliwa na teknolojia ya video
Mtaalam wa teknolojia ya video akiufuatilia mchezo huo kwa umakini



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni