Michy Batshuayi anajiandaa kuondoka
Chelsea katika kipindi cha majira ya joto, iwapo hatoweza
kuhakikishiwa mustakabali wake wa baadae Stamford Bridge ikiwemo
kucheza katika kikosi cha kwanza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
23, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Ufaransa ya Marseille kwa kitita
cha paundi milioni 33.1 hajaanzishwa hata katika mchezo mmoja wa Ligi
Kuu ya Uingereza katika msimu huu.
Mchezaji huyo raia wa Ubelgiji sasa
anataka kuhakikishiwa nafasi ya kuichezea Chelsea katika kikosi cha
Antonio Conte, awali alikuwa anahusishwa na kutaka kuhamia timu ya
West Ham mwezi Januari.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni