.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 30 Julai 2017

DANI ALVES AANZA KWA KUFUNGA GOLI AKIWA NA PARIS ST GERMAIN

Dani Alves amefunga goli katika mchezo wake wa kwanza wakati Paris St Germain ikiwafunga mabingwa wa Ligi 1 Monaco kwa magoli 2-1 na kutwaa kombe la mabingwa.

Katika mchezo huo Djibril Sidibe alikuwa wa kwanza kuziona nyavu na kuifanya Monaco kuongoza baada ya kuubetua mpira na kumshinda kipa Alphonse Areola.

Lakini Alves, aliyenunuliwa akitokea Juventus kwa uhamisho huru mapema mwezi huu alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya 51.

Alves tena alimpikia goli Adrien Rabiot aliyeifungia Paris St Germain goli la pili na kuibuka mabingwa kombe hilo linalojulikana Kifaransa kama Coupe de France.
          Dani Alves akiachia shuti na kufunga goli akiichezea kwa mara ya kwanza PSG
             Dani Alves akibusu kombea la washindi la Coupe de France baada ya kukabidhiwa
              Wachezaji wa Paris St Germain wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni