.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 29 Julai 2017

JUKWAA LA (WAA) LINAWEKA WANAWAKE KATIKA KIINI CHA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA AFRIKA

Jukwaa la WAA (Women Advancing Africa) - limejipanga kukutanisha wataalamu na nguli wa Afrika kutatua changamoto muhimu kwa pamoja na kutengeneza agenda ya kuendesha maendeleo ya kiuchumi ya wanawake Afrika
Tarehe 27 Julai 2017, Dar es Salaam - Maandalizi ya mwisho ya ufunguzi wa Jukwaa la Women Advancing Africa (WAA) yanaendeleayakiwa ni jitihada za Pan Afrika mpya zilizoanzishwa na Graça Machel Trust kutambua na kusherehekea nafasi na ngazi muhimu ambayo wanawake wanaishikilia katika kuleta maendeleo ya Afrika na kuendesha mageuzi ya kijamii na kiuchumi. 

Kongamano litafanyika kuanzia Agusti 9 hadi 12 jijini Dar es Salaam, Tanzania katika hotel ya Hyatt Kilimanjaro.

Akizungumzia kuhusu kwanini taasisi hiyo imeanzisha jukwaa la WAA, Mama Graça Machel amesema “Japo kuwa Afrika imeshuhudia maendeleo makubwa sana katika miongo ya hivi karibuni, pengo kubwa katika maendeleo ya wanawake kiuchumi linabakia kuwa changamoto.

Tuko katika zama zingine za ukombozi – ukombozi wa wanawake kiuchumi. Wanawake hawawezi kutengwa tena na kwa kupitia Women Advancing Africa, Taasisi inataka kuwawezesha wanawake kuchukua nafasi ya muhimu katika kuendeleza uchumi wa Afrika. Taasisi inatoa jukwaa la wanawake kudai haki yao ya kukaa katika meza ambako maamuzi yanafanyika na kubadilisha sera, mipango na mikakati kwa ajili ya baadae na kizazi kijacho”.

Taasisi imepata heshima ya kujiunga kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na mjumbe wa Sekretariet kuu ya Umoja wa mataifa UN wa Jopo la Ngazi ya juu katika Uwezeshaji kiuchumi wa Wanawake (Women’s Economic Empowerment) Samia Sululu Hassan katika jukwaa la WAA, kwaajili ya kutoa mtazamo wake katika masuala ambayo yatajadiliwa katika kipindi cha siku nne cha kongamano hilo. 

Kongamano litakuwa na vipindi vya mahojiano ambavyo vimeandaliwa katika misingi mikuu mitatu. Ujumuishaji wa kiuchumi, Upataji wa masoko na Mabadiliko ya kijamii.

Mchangamano wa rika na mchangamano wa kisekta wa washiriki katika Kongamano la WAA Kwa makadirio ya mahudhurio ya washiriki 200 kutoka barani kote, kongamano la WAA litakusanya pamoja mchanganyiko wa wanawake na vijana watakaowakilisha viongozi na wahamasishaji kutoka katika sekta binafsi, taaluma,taasisi za umma, serikali, taasisi za kimaendeleo na vyombo vya habari ambavyo vitaleta sauti zao, uzoefu wao na mawazo yao kwaajili ya kuweka mikakati, kuweka vipaumbele na kutengeneza agenda ya pamoja katika kuendesha mageuzi ya kijamii na kimaendeleo ya Afrika.

Idadi kadhaa ya wazungumzaji katika sekta muhimu kama vile migodi na uchimbaji, kilimo biashara, Benki, mawasiliano, vyombo vya habari, huduma za afya, bidhaa na huduma wataleta ujuzi na utaalamu wao katika kongamano.

Wazungumzaji mashuhuri watakuwepo wakiwemo Leymah Gbowee mwanaharakati wa kutetea amani wa Liberia na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Vera Songwe Katibu mkuu wa Tume ya Uchumi ya Umoja Wa Mataifa, Dk. Monique Nsanzabaganwa, Gavana Msaidizi wa Benki ya Taifa ya Rwanda, na Sheila Khama, Meneja Mtendaji kwenye kitengo cha Benki ya Dunia cha Sekta ya Madini cha Kimataifa.

Agenda ya Maendeleo ya Jamii

Kutakuwa na mfululizo wa matukio ya pembeni yatakayofanyika sambamba na kongamano la WAA kuhusu masuala mbalimbali ikijumuisha virutubisho na chakula bora, elimu na ndoa za utotoni, uongozi na mazingira bora ya kazi, kuleta umuhimu wa mabadiliko ya kijamii kama kipengele muhimu cha kutazama mwanamke kwa ujumla wake n.k.

Kongamano la WAA pia litasherehekea tamaduni anuai za Afrika na ubunifu katika mifumo yake yote, kuanzia katika Lugha, mpaka katika ubunifu na mitindo, na utengenezaji wa filamu na kucheza ngoma. Kongamano la mwaka huu litasherehekea waandishi na wasimulia hadithi ambao wanatoa changamoto kwa waandishi waliopo, wakiwa wanabadilisha usimuliaji na kutengeneza ujuzi wa kina wakupongezw pamoja na sekta ya viwanda na jukumu lao katika kuendeleza maendeleo ya kijamii.

Utafiti unaotazama katika masimulizi na ushiriki wa wanawake katika uchumi Afrika.

Ripoti mbalimbali zitazinduliwa wakati wa kongamano hilo. Pamoja na Tume ya Uchumi ya umoja wa Mataifa kwa Afrika (United Nations Economic Commission for Africa (UNECA), Graça Machel Trust itazindua uchunguzi kuhusu Uchumi wa mwanamke wa Afrika “The Female Economy in Africa”. 

Utafiti huo utachambua ushiriki wa kazi za wanawake katika Afrika, wakijikita katika uwiano wa kijinsia katika uchumi, ushiriki katika siasa za taifa, ushiriki katika fedha na ubaguzi wa kisekta. Uchunguzi huo utatoa msingi wa namna ya kupima na kufuatilia maendeleo katika shughuli za wanawake wakiwa wanatoa hali halisi katika taarifa zitakazo kuwa zinasambazwa.

Mtandao wa wanawake walioko katika vyombo vya habari wa Graça Machel Trust pia utazindua ripoti ya utafiti kuhusu uwasilishaji wa mwanamke katika vyombo vya habari itakayokuwa inaitwa: women in media - Masimulizi ni yapi?” kipindi hicho kitatangazwa kama kipindi cha moja kwa moja katika mtandao wa Facebook, kutakuwa na ushiriki wa moja kwa moja kwaajili ya kuchochea mazungumzo mapana zaidi kuhusu masimulizi ya mwanamke katika vyombo vya habari pamoja na mifumo mingine ya usimuliaji. 

Tangazo litatolewa katika tovuti ya WAA www.WomenAdvancingAfrica.com na ukurasa wa facebook wa WAA, www.Women Advancing Africa – WAA, muda wake ukikaribia.

Kidokezo kingine katika uzinduzi wa forum ya WAA itakuwa ni uzinduzi wa kitabu (coffee table book) kinachosherehekea juhudi za wanawake katika biashara kikiwa na mkusanyiko wa masimulizi ya kuhamasisha kutoka Botswana, Burundi, Cameroon, Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Senegali, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe. 

 Wanawake watengenezao utajiri: mkusanyiko wa masimulizi ya wanawake wajasiriamali kutoka Afrika nzima. Kitabu hicho kitajumuisha idadi kubwa ya wanawake wanaofanya ujasiriamali kutoka katika mtandano wa wanawake wa taasisi ya Graca Machel Trust na kimewekewa utangulizi na Mama Machel.

Mwenendo wa wanawake waliojikita katika kujiendeleza kiuchumi.
Akielezea nini kinaifanya WAA kuwa ni jukwaa la kipekee, Mama Machel alihitimisha kwamba, “Uendelezaji wa wanawake Afrika unatoa nafasi kuleta pamoja nguvu, uboreshaji na ubunifu wa wanawake kutoka kila pembe ya Afrika kwaajili ya kutoa suluhisho na kutufanya wote tuwe imara, tulioungana na tusioweza kuzuilika.

 Jukwaa hii kweli ni kichochezi katika kutengeneza vuguvugu kubwa zaidi la wanawake waliojikita katika kuendeleza wanawake kiuchumi ambao kwa pamoja wanaijenga na kuiendesha agenda ya maendeleo ambayo itakuwa inapimika na endelevu”. 

Kwa upana wa mtandao wa Pan Afrika ambao unafikia nchi 20, Graça Machel Trust itasaidia kupanua mtandao wa wanawake katika kilimo, biashara na ujasiriamali, fedha na vyombo vya habari kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa WAA kuchochea kongamano hilo kufanikisha utendaji ambao unapimika na matokeo endelevu.

Kuwa sehemu ya jitihada hizi zenye msisimko, unaweza kujiandikisha hapa au kushiriki moja ya maonyesho yake au matukio ya ziada yaliyopo.
Taasisi ya Graca Machel Trust inapenda kuwashukuru wadau wenye roho njema ambao wamewezesha kufanikisha ndoto yao kuwa kweli. Shukurani za pekee ziende kwa UPS Fondation, Intel Foundation, American Tower Corporation na UN Women. Vyombo vya habari washirika ikiwemo: ABN360 Group, ikijumuisha CNBC Africa na Forbes Africa; Nation Group na chombo cha habari cha hapa Tanzania Azam Media Group. APCO Worldwide imefanya kazi kwa karibu sana na taasisi ya Graça Machel Trust, katika kutoa ujuzi na mwongozo kwenye kuunda mtandao huu wa kipekee wa wanawake. Washirika hawa wanakubaliana na imani ya taasisi hii kwamba kumuendeleza mwanamke kiuchumi ni muhimu kwaajili ya maendeleo endelevu ya familia za kiafrika, jamii na taifa.
Imetolewa na:
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Graça Machel Trust: Rosemary Viljoen,
Barua Pepe: RosemaryV@GracaMachelTrust.org
Namba za simu za Maneja Mahusiano wa Vyombo vya Habari APCO: Anthony DeAngelo,
(t) +1.202.778.1000
(m) +1.202.702.7510
Barua pepe: ADeAngelo@APCOworldwide.com

IJUMAA, JULAI 28, 2017

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni