.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Julai 2017

NEYMAR AFUNGA MAGOLI MAWILI NA KUIPA BARCELONA USHINDI

Neymar ameweka kando uvumi wa uhamisho wake kwenda PSG na kuamua kufanya kweli uwanjani kwa kufunga magoli mawili wakati Barcelona ikiifunga Juventus magoli 2-1.

Mchezo huo wa kirafiki umechezwa Jijini New York Marekani katika uwanja wa MetLife ambao tiketi za viti vyote 82,500 ziliuzwa.

Neymar aliipatia Barcelona goli la kwanza baada ya kugongeana vyema na Lionel Messi na kisha kuongeza goli la pili dakika 11 baadaye.

Juventus walipata goli pekee kupitia beki wao mkongwe mwenye uzoefu Giorgio Chiellini aliyefunga kwa mpira wa kichwa.
                   Neymar akiruka juu kushangilia moja ya goli alilifunga dhidi ya Juventus 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni