Mchezaji aliyetokea benchi Olivier
Giroud amefunga goli zuri la ushindi wakati Arsenal wakipambana
kutoka nyuma na kuifunga Leicester City magoli 4-3 katika mchezo wa
kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu wa 2017-18.
Arsenal ilikuwa nyuma kwa magoli 3-2
zikiwa zimebakia dakika saba tu mpira kumalizika kabla ya Aaron
Ramsey na Giroud kubadilisha matokeo ya mchezo huo na kuwafanya
wenyeji kuibuka na ushindi katika dimba la Emirates.
Katika mchezo huo mchezaji mpya wa
Arsenal Alexandre Lacazette alifunga goli la kwanza ndani ya sekunde
94 akishuka mara ya kwanza dimbani katika ligi hiyo lakini Shinji
Okazaki akaisawazishia Leicester City dakika mbili baadaye.
Jamie Vardy aliongeza goli la pili
lililotokana na krosi ya Marc Albrighton kabla ya Danny Welbeck
kufunga goli la kusawazisha. Vardy tena akafunga goli akiunganisha
mpira wa kona uliopigwa na Riyad Mahrez.
Shinji Okazaki akiruga juu na kufunga kwa mpira wa kichwa katika mchezo huo
Mshambuliaji Danny Welbeck akiifungia Arsenal goli
Kipa wa Leicester City, Schmeichel akijaribu bila mafanikio kuzuia mpira wa kichwa uliopigwa na Olivier Giroud
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni