.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 8 Agosti 2017

BARCELONA BILA NEYMAR YAIFUNGA MKONO TIMU YA CHAPECOENSE

Barcelona imeibuka na ushindi mnono dhidi ya timu ya Chapecoense ambayo ilipata ajali ya ndege iliyopelekea vifo vya wachezaji wake na maafisa 71 walipokuwa wakienda kwenye fainali ya kombe la michuano ya Amerika ya Kusini.

Katika mchezo huo waliocheza mara ya kwanza bila ya Neymar aliyesajiliwa na PSG, Lionel Messi na Luis Suarez walifunga huku naye Gerard Deulofeu aliyechukua namba ya Neymar akifunga goli la kwanza katika dakika ya sita kisha Sergio Busquets kufunga la pili.

Lionel Messi alifunga goli la tatu huku Luis Suarez akifunga goli la nne na baadaye Denis Suarez kufunga goli la tano. Katika mchezo huo mchezaji aliyenusurika katika ajali ya ndege Alan Ruschel alicheza kwa mara ya kwanza kwa dakika 35 tangu apate ajali.
         Vikosi vya zimu zote mbili vikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo
Wachezaji wa timu ya Chapecoense walionusurika katika ajali ya ndege wakiwa wenye majonzi dimbani

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni