.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 23 Agosti 2017

VITA BARIDI INAONEKANA KUNUKIA KATIKA KLABU YA BARCELONA

Vita baridi inaonekana kufukuta kati ya bodi ya klabu ya Barcelona na wachezaji kufuatia Lionel Messi kuweka picha yake akiwa na Neymar, baada ya klabu hiyo kutangaza nia ya kumshtaki nyota huyo wa PSG.

Inaonekana kuwa Lionel Messi sasa amebainisha matatizo yaliyopo ndani ya klabu hiyo baada ya kuposti kwenye Instagram yake picha yake hiyo aliyoipiga akiwa pamoja na na Nemyar na Luis Suarez.

Timu ya Barcelona jana ilitangaza kuwa itampeleka Mahakamani Neymar kwa kushindwa kuheshimu kifungu cha kuongeza mkataba na klabu hiyo alichosaini katika mkataba wake alioingia mwaka jana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni