.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Novemba 2017

CHELSEA YASHINDA; CONTE AKILIA NA UGUMU WA RATIBA ZA MECHI

Kocha wa Chelsea Antonio Conte ameviomba vyombo vya habari kumsaidia kuanika ugumu wa ratiba za mechi zinazomkabili wakati klabu yake ikitinga hatua ya 16 bora baada ya kuifunga Qarabag kwa magoli 4-0.

Magoli mawili kutoka kwa Wilian, pamoja na ya mikwaju ya penati ya Eden Hazard na Cesc Fabregas, yalitosha kuithibitishia Chelsea kuweza kumaliza katika nafasi mbili za juu za kundi C huku wakiwa na mchezo mmoja.

Kilio hicho cha Conte kinatokana na kukabiliwa na mchezo dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, Siku ya Jumamosi ikiwa ni siku mbili tu baada ya safari ya umbali wa mile 5,000 kutokea Azerbaijan.
                                        Mchezaji wa Chelsea raia wa Brazil Willian akifunga goli 
                            Kapteni wa Qarabag akionyeshwa kadi nyekundu na kutolewa nje

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni