Mohamed Salah amefunga goli katika
michezo sita mfululizo wakati Liverpool ikiifunga West Ham magoli 4-1
na kukwea juu ya Manchester United katika msimamo wa ligi.
Emre Can alikuwa wa kwanza kukipatia
kikosi hicho cha Jurgen Klopp goli la kwanza kwa mpira wa kona, baada
ya mpira uliopigwa na Salah kugonga mwamba.
Salah alifunga goli la pilibaada ya
kupatiwa pasi tamu na Alex Oxlade-Chamberlain na kisha baadaye
Roberto Firmino akafunga la tatu kwa kosa la kipa Adrian.
Goli zuri la Michail Antonio liliipa
West Ham matumaini lakini Sadio Mane ambaye aligonga mwamba mara
nyingi akapata nafasi ya kutumbukiza mpira kimiani.
Emre Can akiwa amefunga goli la kwanza la Liverpool kwa mpira wa kichwa
Mohamed Salah akifunga goli la pili la Liverpool kwa shuti la mguu wake hatari wa kushoto



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni