Kaimu Mkurugenzi Masoko wa PBZ,Ndg. Seif Suleiman, akionesha moja ya fulana zilizotolewa na PBZ, kwa ajili ya kusherehekea sherehe za kutimia miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg Seif Suleiman, akimkabidhi moja ya fulana 500 zilizotolewa na PBZ kwa Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ndg Haji Ame, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga.
Jumatano, 31 Desemba 2014
KUELEKEA SHEREHE ZA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, PBZ YAKABIDHI FULANA
Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndg, Haji Ame, akitowa shukrani kwa Uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar kwa kukabidhi Fulana mia tano kwa ajili ya sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi hiyo Vuga Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Seif Suleiman, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi fulana 500 kwa ajili ya sare ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar, yatakayoadhimishwa 12,Jan 2015 katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
TATHMINI YA PAPA KAIJAGE KUHUSU MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI KWA MWAKA 2014
•Yamoto Band yazinduliwa rasmi tarehe 21-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.
•Utalii Band yazinduliwa Ijumaa ya tarehe 26-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa MRC (Mikocheni Resort Centre)
•Kundi la Chuchu Sound liliibuka tena na kupiga show kadhaa katika ukumbi wa Max Bar Ilala. Baadaye kwa sababu kadhaa bendi ikapotea.
•Pia kulikuwa na bendi ambazo sio mpya lakini ndani ya mwaka 2014 ziliundwa upya. Bendi hizi ni Victoria Sound na Ruvu Stars.
•Bendi nyingine zilizoanzishwa ndani ya mwaka 2014 ni JJ Band, bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe. Pia kuna Ruby Band. Bendi hizi 2 zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2015.
UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Extra Bongo walizindua album ya “Mtenda Akitendewa” Jumamosi ya tarehe 22-Feb-2014 ndani ya Dar Live Mbagala.
•Talent Band (ya Hussein Jumbe) wazindua album ya “Kiapo Mara Tatu” Jumatano ya 30-Apr-2014 ndani ya Kisuma Night Pub, Temeke (zamani Sugar Ray)
•Christrian Bella azindua album ya “Nani Kama Mama” ndani ya Mzalendo Pub Jumamosi ya tarehe 30-Aug-2014
•Tarsis Masela katika viunga vya Ten Lounge (Business Park) Victoria azindua album ya “Acha Hizo” Ijumaa ya tarehe 21-Nov-2014
•Mashujaa Band yazindua album ya “Ushamba Mzigo” kwenye ziara za mikoani.
KILI MUSIC AWARD
•Kili Music Award 2014 ilifanyika Jumamosi ya tarehe 03-May-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 8 vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu)
2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta)
3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band)
5. Bendi Bora-Mashujaa Band
6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band)
7. Producer Bora-Amorosso
8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra)
WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed “MCD” afariki dunia Jumatatu ya tarehe 27-Jan-2014
•Mpiga bass wa Vijana Jazz, Maulid Mwangia afariki Jumatano tarehe 12-Mar-2014 na kuzikwa Alhamis tarehe 13-Mar-2014
•Mwanamuziki mkongwe Muhiddin Gurumo afariki dunia Jumapili ya tarehe 13-Apr-2014 na kuzikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe Jumanne ya tarehe 15-Apr-2014
•Mpiga gitaa wa Skylight Band, Chili Challa wa Skylight Band afariki dunia tarehe 17-Apr-2014.
•Amina Ngaluma “Japanese” afariki tarehe 15-May-2014 akiwa mji wa Phuket, Thailand.
•Mwanamuziki DIGITAL wa FM Academia afariki Ijumaa tarehe 18-Jul-2014.
•Ally Rashid “Mwana Zanzibar” ambaye mara ya mwisho alikuwa mpuliza sax wa Msondo Ngoma afariki tarehe 10-Oct-2014.
•Suzuki Sauti ya Malaika aliyepigia Extra Bongo katika album ya “Mjini Mipango” alifariki tarehe 15-Oct-2014
•Mwanamuziki Khamis Kayumba “Amigoulaus” afariki tarehe 09-Nov-2014.
•Mwanamuziki Shem Ibrahim Kalenga afariki dunia 15-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 16-Dec-2014 katika makaburi ya Kisutu.
•Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia tarehe 17-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 19-Dec-2014.
MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Mdahalo wa kwanza wa aina yake wa kujadili muziki wa dansi wafanyika katika ofisi za TBC Jumamosi ya tarehe 05-Apr-2014 chini ya u-moderator wa Dacota Khamis, kuhudhuriwa na wadau karibia 30 na kuonyeshwa live na TBC2 na baadaye kuonyeshwa recorded na TBC1 kwenye kipindi cha “Nyumbani ni Nyumbani”
•Bendi ya Msondo Ngoma yafanya sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 50. Maadhimisho yalianza Ijumaa ya tarehe 10-Oct-2014 ndani ya Leaders Club na kuhitimishwa TCC Chang’ombe Jumamosi ya tarehe 01-Nov-2014. Pia wanamuziki wa bendi walikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, Alhamis ya tarehe 30-Oct-2014.
•Kwa mara ya kwanza tukio la “Usiku wa Msanii” lafanyika tarehe 25-Oct-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Marehemu Father Kanuti alipewa tuzo ya Humanitarian Award.
•Tarehe 09-Dec-2014, siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru na miaka 52 ya Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla maalum iliyofanyika katika viwanja vya ikulu atoa nishani maalum kwa kundi zima la Atomic Jazz Band ya Tanga. Tuzo hiyo ni ya miaka 50 ya Muungano ya daraja la nne. Aliyepokea kwa niaba ya kundi ni mzee Stephen Hiza (Mgosingwa). Atomic Jazz Band imepewa nishani hiyo kutokana na kazi yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi muungano hususan kwa kupitia wimbo wao wa “Tanzania Yetu”.
•Mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika mara mbili kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment. Mara ya kwanza ulifanyika siku ya sikukuu ya Eid Mosi (Eid al-Fitr) tarehe 25-Jul-2014 ndani ya TCC Chang’ombe. Mara ya pili umefanyika pia TCC Chang’ombe Christmas tarehe 25-Dec-2014. Kwenye mpambano wa mara ya pili, kwa mara ya kwanza tukio limesindikizwa na bendi ya Vijana Jazz Pambamoto “Saga Rumba”.
•MAONYESHO YA PAMOJA: Bendi 3 za FM Academia, Mapacha Watatu na Ruby Band zapiga pamoja Ijumaa ya tarehe 19-Dec-2014 ndani ya Mzalendo Pub. Yamoto Band mara kadhaa imefanya maonyesho ya pamoja kwa kupiga pamoja na Mapacha Watatu, Skylight Band na Twanga Pepeta. Pia Mlimani Park Orchestra wamepiga pamoja mara kadhaa na Machozi Band ya Lady Jaydee. Ruby Band walipiga pamoja na Twanga Pepeta Jumapili ya tarehe 28-Dec-2014 ndani ya Leaders Club
•Onyesho la Miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta lililokuwa lifanyike Jumamosi ya tarehe 20-Dec-2014 limeahirishwa hadi tarehe 31-Jan-2015 kutokana na kifo cha mnenguaji Aisha Madinda.
•Mechi ya mpira wa miguu kati ya kundi la BONGO DANSI na kundi la WATANASHATI WA MUJINI lafanyika katika viwanja vya Leaders Club Jumapili ya tarehe 23-Nov-2014. Matokeo yalikuwa suluhu 0-0. Kundi la BONGO DANSI mara kadhaa limefanya ziara ya kumtembelea Nguza Vicking na Papii Kocha ambao wapo gerezani Ukonga.
•Tarehe 26-Dec-2014, umoja wa wanamuziki wa dansi katika viwanja vya Karimjee wafanya dua maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete ili hali yake ya kiafya iimarike.
SSRA EMERGED AN OVERALL – ATE WINNER UNDER THE CATEGORY OF WORKFORCE FOCUS
In a jovial mood the Director General of SSRA,Irene Isaka receiving a certificate of participation from the Prime Minister Hon. Mizengo Peter Pinda during the Employer of the year Award, where SSRA emerged an overall winner under the category of Workforce Focus. From left is Ms. Zuhura Muro Vice Chairperson of Association of Tanzania Employers (ATE); Hon. Gaudentia Kabaka Minister for Labour and Employment; on right is Mr. Almasi Maige ATE Chairperson.
Very proud with her team the Director General Mrs. Irene Isaka holding a trophy as an overall winner of the Employer of the year Award under the category of Workforce Focus. On left is Ms. Lightness Mauki Director of Compliance and Registration.
SSRA members of Staff celebrate by holding the trophy from left; Ms. Beatrice Ngong’ho, Ms.Husna Lukosi, Mr. Simon Aikambe and Mr. Innocent Kyara.
Director General of SSRA Mrs. Irene Isaka with her team posing for a group photo after emerging the overall winners of the Employer of the year Award under the category of Workforce Focus 2014. Holding the Trophy is Mr. Ansgar Mushi Director of Research, Actuarial and Policy analysis.
Posing with his team holding trophy is Human Resource and Administration Manager Mr. Teophory Mbilinyi.
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AHUTUBIA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba yake fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Magereza, Mmeta Manyala.
Baadhi ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(katikati) mara baada ya kutoa hotuba fupi katika Baraza la kufunga Mwaka 2014 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2015.
Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu Watumishi wenzao ambao wametangulia mbele ya haki kwa mwaka huu 2014.SALAAM ZA MWAKA MPYA WA 2015 TOKA KWA RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za mwaka mpya wa 2015 kwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na kuwatakia mwaka wenye Amani na Utulivu pia mafanikio makubwa ikiwemo ya Uchumi wa Taifa letu. Hafla hiyo ilifanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja [Picha na Ikulu.]
MIILI YA KWANZA YA WALIOKUFA KWA AJALI YA NDEGE YAWASILI SURABAYA
Miili miwili ya kwanza kutoka ndege
ya AirAsia namba QZ8501 iliyoanguka imewasili katika mji wa Surabaya
nchini Indonesia ambako ndugu wanangojea.
Ndugu wa karibu wameomba kufanyiwa
vipimo vya DNA, ili kusaidia kubaini miili ya ndugu zao waliokufa.
Ndege hiyo aina ya A320-200, ikiwa
na abiria 162 wakitokea Surabaya kwenda Singapore, ilitoweka siku ya
jumapili, na mabaki yake kuonekana baharini siku ya jumanne.
Mamlaka ya Indonesia imesema miili
saba zaidi imeopolewa, lakini zoezi hilo limeathiriwa mno na hali
mbaya ya hewa.
Miili hiyo ikiwa imebebwa kwenye majeneza yaliyopewa namba 001 na 002
Awali miili hiyo ilisafirishwa kwenye mifuko ya plastiki kutoka baharini hadi katika uwanja wa ndege wa karibu wa jeshi, na kisha kuwekwa kwenye majeneza ya mbao.
MTUNZI MKONGWE WA VITABU, BI FATMA MOHAMED SALIM ( JINJA ) AZINDUA VITABU VYA HADITHI ZA KALE
Mtunzi mkongwe wa vitabu Zanzibar Bi. Fatma Moh’d Salim (Jinja) akionyesha vitabu vya hadithi za kale alivyovitunga, katika sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo zilizofanyika nyumbani kwake Chukwani Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Mwandishi wa Habari wa Redio Annur Fm Kasim Khamis akimuuliza swali Bi. Fatma Jinja kuhusiana na utunzi wa vitabu vyake alivyo vizindua.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo wakimskiliza Bi. Fatma Jinja (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo juu ya utunzi wa vitabu hivyo .
Mwandishi wa Habari wa Redio Annur Fm Kasim Khamis akimuuliza swali Bi. Fatma Jinja kuhusiana na utunzi wa vitabu vyake alivyo vizindua.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa vitabu hivyo wakimskiliza Bi. Fatma Jinja (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo juu ya utunzi wa vitabu hivyo .
Waandishi wa Habari wakifanya mahojiano na mtunzi wa vitabu Bi. Fatma Jinja huko nyumbani kwake Chukwani Zanzibar baada ya uzinduzi wa vitabu vyake. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
WAFANYAKAZI WA PPF IDARA YA UENDESHAJI WAFANYA SHEREHE YA KUFUNGA MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM JANA
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Assumpta Maina Mallya akifungua sherehe iliyoandaliwa na idara yake kwaajili ya kupongezana kwa kazi za mwaka mzima, sherehe iliyofanyika katika hoteli ya Tiffany jijini Dar Es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka idara ya Uendeshaji wakimsikiliza Kwa Makini Mkurugenzi wa Idara hiyo wakati akifungua Sherehe ya Kupongezana kwa Wafanyakazi wa Idara hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Tiffany, Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akikata keki kwaajili ya Kuwarisha wafanyakazi wa Idara yake katika Sherehe ya kufunga mwaka iliyoandaliwa na Idara ya uendeshaji na kufanyika katika hoteli ya tiffany Jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Assumpta Maina Mallya akimlisha Keki mmoja wa Wafanyakazi wa Idara hiyo.
SERKALI YAOMBWA KULINDA BEI ZA FILAMU NCHINI
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel aliyesimama akifungua Mkutano Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini (hawapo pichani)kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu, wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini. Bi. Joyce Fissoo.Mkutano huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fissoo aliyasimama akifafanua jambo kwa wadau wa usambazaji wa Filamu nchini wakati wa Mkutano wa Baina yao na Serikali uliofanyika jijini Dar es Salaam,wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mwanasheria wa Wizara Bw. Patrick Kipangula.Baadhi ya wasambazaji wa Filamu nchini wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Olegabriel (hayupo pichani) akifungua Mkutano wa wasambazaji wa Filamu nchini kuhusu kuporomoka kwa bei ya filamu. Mkutano huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Benjamin Sawe)
MTUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA APIGWA RISASI NA KUFA AKIJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU
Mtuhumiwa wa dawa za kulevya Adul
Koroma raia wa Sierra Leone amepigwa risasi na kufa wakati akijaribu
kutoroka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka
leo asubuhi alipofikishwa Mahakamani kwa ajili ya kutajwa kesi yake,
ambapo aliwatoroka askari na kukimbia kupanda fensi ya chuma na nguo
zake zilinasa kwenye vyuma na polisi kumuwahi kwa kumpiga risasi.
Watu wakishanga baada ya mtuhumiwa huyo kupigwa risasi
Askari Magereza wakiutoa mwili wa mtuhumiwa aliyeuwawa
MTOTO WA MIAKA MIWILI AMPIGA RISASI MAMA YAKE MZAZI NA KUMUUA NCHINI MAREKANI
Mwanamke mmoja katika jimbo la Idaho
nchini Marekani ameuwawa na mtoto wake wa kiume wa miaka miwili kwa
kumpiga risasi baada ya kuchukua bastola kwenye pochi yake.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa
jina la Veronica J Rutledge, mwenye umri wa miaka 29, alipigwa risasi
na mtoto wake huyo kwenye duka la Wal-Mart katika mji Hayden.
Msemaji wa duka hilo amesema
mwanamke huyo alikuwa anafanya manunuzi akiwa na watoto kadhaa wakati
wa tukio hilo. Maafisa wamesema marehemu kibali chake cha silaha
kilikuwa kimefutwa.
RAPA KANYE WEST AUNGA MKONO IDRIS ELBA KUWA JAMES BOND WA KWANZA MWEUSI
Mjadala unaokuwa kwa kasi iwapo
Idris Elba awe muigizaji wa kwanza mweusi kuigiza nafasi ya James
Bond, umeonekana kuungwa mkono na mmoja wa rapa maarufu wa Marekani
Kanye West.
Rapa huyo muongeaji mno, amesisitiza
kuwa Idris ni chagua sahihi kuchukua jukumu la kumbadili Daniel
Craig, na kazi hiyo itakuwa ni ya maono makubwa.
Kanye ameliambia gazeti la The Sun,
kuwa anamjua Idris kiasi na ni mtu mwenye kipaji kikubwa cha
uigizaji, na filamu alizoigiza ni kali na jukumu la James Bond likija
yeye anafaa.
James Bond wa sasa Daniel Craig
RAIS WA GAMBIA ASEMA BADO ANASHIKILIA MADARAKA YA NCHI HIYO BAADA YA JARIBIO LA KUMPINDUA
Rais wa Gambia amesema bado
anashikilia mamlaka na taifa hilo la Afrika Magharibi, baada maafisa
usalama wake kuzima jaribio la kumpindua.
Rais Yahya Jammeh amesema kamanda wa
zamani wa jeshi alitaka kutwaa madaraka ya nchi hiyo kwa nguvu wakati
akiwa ziarani nchini Ufaransa, hata hivyo hatma ya kamanda huyo
haijulikani.
Awali kulikuwapo na milio mizito ya
risasa karibu na Ikulu ya rais huyo katika mji mkuu.
Rais Jammeh alitwaa madaraka ya
Gambia kwa mapinduzi mwaka 1994, na wakosoaji wake wanamlaumu kwa
kuiongoza nchi hiyo kwa utawala wa mkono wa chuma.
WATU WAZIMA SABA NA WATOTO WAWILI WAKUTWA WAKIWA WAMEKUFA CANADA
Mmoja wa waliyekufa inaaminika kuwa
amejiua mwenyewe, na polisi hawana nia ya kumtafuta mtuhumiwa na
wanachukulia mauji hayo kuwa ni ya mgogoro wa kifamilia.
Mauaji hayo yamefanyika katika
maeneo tofauti ya mji wa Edmonton, kwenye mkoa wa magharibi wa
Alberta na miili saba imekutwa kwenye nyumba moja mkuu wa polisi Rod
Knecht amesema.
FLYBE YATUA KWA DHARURA IKIWA NA ABIRIA 69
Ndege ya shirika la ndege la Flybe ikiwa na abiria 63 imelazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Belfast baada ya kuwepo kwa harufu ya moshi kutoka katika sehemu ya kubeba mizigo ya ndege hiyo.
WAZIRI MKUU MSTAAFU, MH EDWARD LOWASSA AMTEMBELEA SUKWA SAID SUKWA NYUMBANI KWAKE MJINI UNGUJA
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali, nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kulia) akifurahia jambo na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi. Kushoto ni Mke wa Sukwa, Fatma Mussa.
RATIBA YA MICHUANO YA KOMBE LA MAPINDUZI YATOLEWA, SIMBA KUANZA NA MTIBWA, AZAM NA KCC WAKATI YANGA KUKUTANA NA VILLA
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Abdalla Said akizungumza na waandishi wa habari wa michezo Zanzibar kwa kukamilika kwa Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi linalotarajiwa kutimua Fumbi Januari 1, 2015 katika Uwanja wa Amaan Zanzibar na kuzitaja timu zitakazoshiriki michuano hiyo.
Amezitaji timu hizo sita kutoka nje ya Zanzibar na sita kutoka Zanzibar na kusema kutakuwa na makundi matatu kila kundi litakuwa na timu Nne.
Amezitaji timu hizo sita kutoka nje ya Zanzibar na sita kutoka Zanzibar na kusema kutakuwa na makundi matatu kila kundi litakuwa na timu Nne.
Amezitaja timu hizo kuwa ni Yanga, Simba,Azam,Mtibwa Sugar kutoka Tanzania Bara na KCC, na Sport Club Villa zote kutoka Uganda,
Timu za Zanzibar zitakazoshiriki michuano hiyo KMKM, Mtende Ranger, Shaba,Polisi,JKU na Mafunzo kutoka Zanzibar. Ameyataja makundi na timu zake.
Alhamis 1 Januari 2015
Jioni Saa 9:00 JKU vs MAFUNZO. -- KUNDI. C
Jioni Saa.11:00. POLISI VS SHABA. KUNDI . A
Usiku Saa 2:15. SIMBA VS MTIBWA. KUNDI C
Ijumaa 2 Jan 2015
Jioni saa 10:00 KMKM VS MTENDE KUNDI B
Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM. KUNDI B
Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA KUNDI C
Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA KUNDI A
MABONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA COSMAS CHEKA KUGOMBANIA MKANDA WA U.B.O AFRICA FEB 28
Mabondia Cosmas Cheka kushoto akitunishiana misuli na Ibrhahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika feb 28 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BOXING NEWS
Jisajili kwenye:
Machapisho
(
Atom
)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

















